Friday, September 21, 2012

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA ZIARA RASMI YA RAIS KIKWETE NCHINI KENYA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete na mwenyeji wao Rais Mwai E. Kibaki baada ya kuwasili nchini Kenya, Jumanne, 11 Septemba , 2012,  kuanza Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ikiwa ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, akitembelea Taasisi ya Utatifi wa Kilimo ya Kenya (KARI).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakipanda miti wakati walipozuru mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia mvuke utokao chini ya ardhi wakati wa  Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu  nchini Kenya.
(PICHA NA IKULU)

No comments:

Post a Comment