Tuesday, October 16, 2012

MTOTO WA KIGOGO AMCHIMBA MKWARA IZZO B


RAPA mwenye swaga, Emmanuel Bryson Simwinga ‘Izzo B’, sasa hivi anaweweseka baada ya mtu aliyejitambulisha kuwa mtoto wa kigogo mmoja wa serikali, kuandika ujumbe mtandaoni akisema atamrudisha Mbeya.
Siyo stori kwamba Izzo kwa sasa anatamba na wimbo “Utarudishwa” ambao amemshirikisha mbishi wa nyimbo za mapenzi, Belle 9 anayeimba “Izzo Izzo Utarudishwa Mbeya” halafu rapa huyo anajibu “Na nani?”
Emmanuel Bryson Simwinga ‘Izzo B’.
Wiki iliyopita, mtoto wa kigogo mmoja serikalini (jina tunalo), aliandika kwenye ukurasa wake katika mtandao wa kijamii, Facebook kuwa Izzo Business tutakurudisha Mbeya.
Baada ya Izzo kuona meseji hiyo, alianza kuweweseka kwa kuzungumza na marafiki zake kwa hisia kwamba baada ya kutoa wimbo huo, zipo njama za kumfanyia kweli ili akaishi kwenye Jiji la Kijani (Green City) ambako ndipo asili yake ilipo.
Showbiz baada ya kutonywa na rafiki wa Izzo, iliamua kuzungumza moja kwa moja na mhusika ambaye alijibu: “Ni kweli hii imetokea, nimejaribu kuwataarifu marafiki zangu kadhaa kiusalama tu, ila mimi siogopi, muziki wangu ni harakati na mwanaharakati hatakiwi kuogopa.
“Hata nilipoimba Utarudishwa ni kwa sababu najua muziki wangu unagusa maslahi ya watu, kwa hiyo sipendwi na wale ninaowatibulia ila Watanzania wengi wapo na mimi. Huyo mtoto wa kigogo kama kweli amedhamiria kunirudisha Mbeya, hebu ajaribu tuone.”

No comments:

Post a Comment