Friday, December 21, 2012

RAIS KIKWETE AKABIDHIWA HATI YA BIMA YAKE YA MAISHA IKULU


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipitia hati ya bima yake ya maisha baada ya kukabidhiwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa Bw. Justine Mwandu jana Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiushukuru uongozi wa  Shirika la Bima la Taifa baada ya kupokea hati ya bima yake ya maisha jana Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea kitabu cha kumbukumbu ya miaka 50 ya Shirika la Bima la Taifa toka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wake Bw. Justine Mwandu jana Ikulu jijini Dar es salaam. Shirika hilo ambalo limefufuka upya linaadhimisha miaka 50 ya kuanzishwa kwake mwakani.
(PICHA NA IKULU)

No comments:

Post a Comment