Bao la Zinedine Zidane wakati wa mchezo huo.
(PICHA ZOTE NA AFP/GETTY IMAGES)
MCHEZAJI mahiri aliyekuwa akiichezea timu ya Taifa ya Ufarans,a Zinedine Zidane, jana alifunga bao safi wakati timu yake ikilala bao 3-2 dhidi ya timu ya gwiji wa soka wa Brazil, Ronaldo de Lima.
Wachezaji hao walikutana jana usiku nchini Brazil katika mechi ya kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia miradi ya kupunguza umasikini nchini Brazil na Afrika iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) ambapo refarii wa mchezo huo alikuwa Pierluigi Collina. Mabao ya kikosi cha Ronaldo yaliwekwa kimiani na Bebeto, Cacá Ferrari na Leandro Damião wakati ya timu ya Zidane yakifungwa na Falcão na Zidane mwenyewe.
Zidane alikuwa nahodha katika timu yake iliyokuwa chini ya kocha Luiz Felipe Scolari ikiundwa na wachezaji Vitor Baía, Juliano Belletti, Diego Cavalieri, Emerson, Fernando Hierro, Míchel Salgado, Fernando Couto, Juan Pablo Sorín, Paolo Montero, Carlos Gamarra, Hidetoshi Nakata, Zinédine Zidane, Deco, Santiago Solari, Fredrik Ljungberg, Juan Román Riquelme, Christian Karembeu, Alex de Souza, Pedro Pauleta, Sebastián Abreu, Hulk, Falcão, Mário Jardel.
Timu ya Ronaldo iliyokuwa chini ya kocha Carlos Alberto Parreira iliundwa na wachezaji : Danrlei, Dida, Cafú, Serginho, Réver, Junior Baiano, Roque Junior, Roberto Carlos, William, Lucas, Juninho Paulista, Zinho, Djalminha, Roger, Zico, Denilson, Ronaldo, Neymar, Leandro Damião, Bebeto, Cacá Ferrari, Romário, Edmundo, Paulinho.
No comments:
Post a Comment