Thursday, January 10, 2013

DP, CCK, UMD NAO WAWASILISHA MAONI YAO TUME YA MABADILIKO YA KATIBA


  Mwenyekitiwa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila akizungumza katika mkutano uliofanyika jana katika Ofisi za Tume hiyo Jijini Dar es Salaam na Chama hicho kilipowasilisha maoni yao Kuhusu Katiba Mpya mbele ya Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakiongozwa na Jaji Joseph Warioba. Kulia ni Katibu wa Tume, Assaa Rashid na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba.
  Mwenyekitiwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akizungumza na Viongoziwa Chama cha Democratic (DP) wakiongozwa na Mwenyekiti wao Mchungaji Christopher Mtikila (kushoto) walipofika katika Ofisi za Tume leo Jijini Dar es Salaam kuwasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya. Katikati ni Katibu wa Tume, Assaa Rashid.
 Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk. Salim Ahmed Salim (wa pili kushoto) akizungumza katika mkutano na Viongozi wa Chama cha Kijamii (CCK) uliofanyika katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam wakati Chama hicho kilipowasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya jana.
 Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Eather Mkwizu (kulia) akizungumza katika mkutano na Viongozi wa Chama cha Kijamii (CCK) uliofanyika katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam wakati Chama hicho kilipowasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya jana.
 Mwenyekiti wa Chama cha Kijamii (CCK), Constantine Makitanda akizungumza katika mkutano uliofanyika katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba mara baada ya  Chama hicho kuwasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya jan.
Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Union for Multiparty Democracy (UMD) wakifuatilia mkutano baina yao na Tume ya Mabadiliko ya Katiba jana, ambapo Uongozi wa Chama hicho uliwasilisha maoni yao ya Katiba Mpya.
(Picha na Tume ya Mabadiliko ya Katiba)

No comments:

Post a Comment