Airtel, Baraza la Taifa la Usalama barabarani waungwa mkono na wananchi
Baadhi ya wananchi wanaoishi jijini Dar es salaam wamesema uamuzi uliofikiwa na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani wa kumtangaza aliyekuwa mpiga picha wa magazeti ya serikali Bw. Athmani Hamisi kuwa balozi wa kampeni ya usalama barabarani una maana kubwa sana.

Wananchi hao wameyasema hayo katika nyakati tofauti walipokuwa wakiojiwa na mwandishi wetu juu ya kampeni hii ya nenda kwa usalama barabarani inayodhaminiwa na Kampuni ya mitandao ya simu za mkononi ya Airtel.
Wananchi wengi wamesema uamuzi huo wa kumteua Bw. Hamisi kuwa Balozi wa kampeni hiyo kwa dhumuni la kutoa elimu ya usalama barabarani utakuwa na matunda zaidi kwa sababu kupitia yeye watu watajifunza vyema juu ya athari za ajali barabarani.

“Kumtumia mtu ambaye alishakuwa muhanga wa ajali ni jambo sahihi kabisa kwa sababu ataweza kutoa ushuhuda wa wazi ni jinsi gani ajali zimemkwamisha hata kwenye shughuli zake za kimaendeleo na kuwaasa vyema watu wanavyotakiwa kujikinga na ajali hizo.” Alisema Calisti Mushi mkazi wa Temeke jijini Dar es salaam.
Kwa upande mwingine baadhi ya wakazi wa sehemu mbalimbali za jiji la Dar es salaam walisema ni kweli kuwa jukumu la kupinga ajali ni la kila mwananchi lakini elimu zaidi inapaswa kutolewa ili kuzitokomeza kabisa.
“Bado elimu inahitajika zaidi kwa watumiaji wa vyombo vya moto ili kuepusha ajali ambazo hutokea kila siku, na kwa kutumia wahanga wa ajali kama Bw. Hamisi watu wataelewa vizuri zaidi ni jinsi gani ajali hudumaza maendeleo ya taifa kiujumla” walisema baadhi ya wananchi waishio katika jiji la Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment