Monday, November 11, 2013

NANE WAFARIKI KATIKA AJALI KENYA


Taswira baada ya ajali hiyo. (Picha: KRCS).
WATU nane wamepoteza maisha katika ajali ya barabarani baada ya lori lililokuwa limebeba mbao kugongana na basi eneo la Sachangwan jirani na njia panda ya Eldoret-Nakuru nchini Kenya!
Wanne kati yao walipoteza maisha papo hapo katika eneo hilo ambalo hutokea ajali mara kwa mara.
Kwa mujibu wa Shirika la Msalaba Mwekundu nchini humo, idadi kamili ya majeruhi katika ajali hiyo bado haijafahamika kwa sasa maana majeruhi wengi wamekimbizwa katika hospitali mbalimbali baada ya ajali hiyo

No comments:

Post a Comment