WENYEJI wa Kombe la Dunia 2014, Brazil wametoka suluhu na Mexico katika mechi yao ya pili ya kundi A. Brazil na Mexico wote kwa sasa wana pointi nne baada ya kucheza mechi mbili kila mmoja.
Mechi ya kwanza Brazil alimpiga Croatia mabao 3-1 wakati Mexico akimchapa Cameroon bao 1-0. Brazil anaongoza kundi hilo kwa tofauti ya mabao.
Katika mechi hiyo, kipa wa Mexico, Guillermo Ochoa ameibuka nyota wa mchezo.
No comments:
Post a Comment