Wednesday, October 10, 2012

NAIBU MKURUGENZI OFISI YA WAZIRI MKUU ATEMBELEA BANDA LA VODACOM KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA HUDUMA ZA KIFEDHA


Mkuu wa Ukuzaji Biashara ya M-Pesa wa Vodacom Tanzania, Jackson Kiswaga akimkabidhi mkurugenzi msaidizi wa ofisi ya waziri mkuu Ezamo Maponde zawadi ya Modem ya Intanet wakati wa uzinduzi wa wiki ya Huduma za kifedha kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi msaidizi wa ofisi ya waziri mkuu Ezamo Maponde akifurahia zawadi ya Modem ya Intaneti aliyokabidhiwa na Mkuu wa Ukuzaji Biashara ya M-Pesa wa Vodacom Tanzania,Jackson Kiswaga wakati wa uzinduzi wa wiki ya Huduma za kifedha kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Ukuzaji Biashara ya M-Pesa wa Vodacom Tanzania, Jackson Kiswaga akitoa maelezo kwa mkurugenzi msaidizi wa ofisi ya waziri mkuu Ezamo Maponde na kumkabidhi zawadi ya Modem ya Intaneti wakati wa uzinduzi wa wiki ya Huduma za kifedha kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom wakitoa maelezo kwa wateja waliohudhuria uzinduzi wa wiki ya Huduma za kifedha kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
---
Taarifa kwa vyombo vya habari
M-pesa yazidi kukubalika sokoni
·         Idadi ya wateja wa kila siku sasa yafikia 3Milioni, Yazungusha Sh 35 Bilioni kwa Mwezi
·         Yatumika na Mashirika mbalimbali kurahisisha huduma
Dar es salaam. 10 Oktoba, 2012. …Huduma ya Vodacom M-pesa imeendelea kuonesha umahiri na kukubalika sokoni na hivyo kuongeza kiwango cha watumiaji mmoja mmoja na kwa makampuni ya kibiashara na maendeleo hapa nchini.
Hadi sasa huduma ya M-pesa imefikisha wateja zaid ya milioni tatu wanaofanya miamala ya manunuzi ya bidhaa na huduma sanjari na kutuma na kupokea pesa kila siku.
Kukua kwa kiwango cha matumizi ya huduma ya M-pesa iliyoanzishwa mwaka 2008 kunaenda sambamba na namna ambavyo huduma hiyo invyokidhi mahitaji ya kila siku ya wanananchi hapa nchini na hata kimataifa kwa usalama, uhakika, urahisi.”M-pesa ni huduma ya malipo ya kuaminika zaidi kwa Watanzania wakiwemo wasiofikiwa na huduma za kibenki.” Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Rene Meza
Rene amesema katika azma ya kurahisisha na kuwezesha malipo katika biashatra mbalimbali pamoja na kuunganisha makampuni yanayotoa huduma na wateja wao, huduma ya M-pesa imevutia ubia na makampuni mbalimbali ambayo kwao imekuwa fursa nzuri zaidi ya kurahisisha utoaji wa huduma na hata kuwa karibu na wateja wao.
“Tumeingia ubia na makampuni mengi yanayotoa huduma tofauti nchini kama vile CRDB, TANESCO, Precision Air, Heritage pamoja na mifuko ya hifadhi ya jamii na makampuni mengine mbalimbali hii yote ni kuhakikisha tunakuwa kiunganishi kati ya watoa huduma na wananchi lengo likiwa ni kuwawezesha wananchi kuwa na maisha rahisi na kuokoa muda” Aliongeza Rene
Mkurugenzi Mtendaji huyo alikuwa akizungumzia wiki ya huduma za kifedha nchini iliyoanza leo viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam na kuanisha kuwa huduma ya M-pesa hufanya miamala yenye dhamani ya zaidi ya Shilingi 35 Bilioni kwa siku. “Tunajivunia hatua hii kutokana na ukweli kwamba inadhihirisha kuwa ni huduma salama, bora, ya kuaminika na ya uhakika inayopatikana kote nchini..
Katika kipindi cha wiki moja huduma ya M-pesa imeingia ubia na kampuni ya Bima ya Heritage kupitia huduma ya Faraja ambapo sasa mwananchi wanauwezo wa kujiandikisha na kulipia huduma za bima pamoja na kupokea fidia ya bima kupitia M-pesa popote walipo wakati wowote, huku ikiingia pia ubia na WFP (Mpango wa Chakula wa Umoja wa Mataifa) kwenye mradi wake wa uwezeshaji wanawake wajawazito lishe bora mkoani Mtwara ambao walengwa watakuwa wakipokea fedha hizo kupitia M-pesa.
“Ubia wote huu unaleta ukombozi kwa wananchi na ni wa aina yake hapa nchini ukidhihirisha ubora wa mtanadao mpana wa M-pesa nchini, mathalani  Faraja Bima mfumo huu wa malipo ya bima kupitia simu ya mkononi haupo popote kwengine dunia zaidi ya Tanzania kupitia M-pesa ni wa kwanza duniani kote, haya ni mafanikio ya kujivunia ya M-pesa.” Alisema Rene  
Wiki ya huduma za kifedha ni tukio la kila mwaka lenye lengo la kutoa elimu na kuwajengea ufahamu  na uelewa wananchi, wafanyabiashara na wadau wengine juu ya ya masuala ya fedha na namna bora ya kusimamia fedha, matumizi na maamuzi ya kifedha kukidhi mahitaji.
Kampuni  ya  Vodacom Tanzania
Kampuni ya Vodacom Tanzania Limited ina dhamira ya dhati ya kushirikiana na  jamii katika shughuli za maendeleo kupitia taasisi yake ya Vodacom Foundation.   Vodacom Foundation  ina nguzo kuu tatu: Afya,  Elimu na Ustawi wa Jamii. Hadi  sasa taasisi hiyo  imechangia zaidi ya miradi 120 ya kijamii nchini. Aidha,  imeshinda tuzo mbalimbali za kitaifa na za kimataifa katika nyanja ya Uwajibikaji wa Mashirika kwa Jamii. Hizi ni pamoja na East African CSR Awards na Diversion and Inclusion Award ambayo hutolewa  na kampuni mama ya Vodafone  .
Vodacom Tanzania Limited ni kampuni ya simu za mikononi inayoongoza Tanzania inayotumia  teknolojia ya kisasa  ya  mawasiliano. Vodacom Tanzania ni kampuni tanzu ya Vodacom Group (Pty) Limited, South Afritca, ambayo pia ni kampuni tanzu ya Vodafone Group UK. Vodacom Group (Pty) Limited inamiliki  hisa ailimia 65 Vodacom Tanzania na  asilimia 35 zilizobaki zinammilikiwa na Mirambo Ltd.
Vodacom Tanzania imetangazwa kuwa  Super Brand (Chapa Bora Zaidi)  kwa miaka  mitatu mfululizo, kutoka 2009 -2011.

No comments:

Post a Comment