Wednesday, December 12, 2012

PAPA BENEDICT XVI 'ATWEET' KWA MARA YA KWANZA AKIWABARIKI WAFUASI WAKE


Papa Benedict XVI akituma ujumbe wake wa kwanza katika mtandao wa kijamii wa Twitter leo mjini Vatican.
Papa Benedict XVI akionyeshwa ujumbe wake alioutuma katika mtandao wa Twitter leo.
Ujumbe wa kwanza wa Papa Benedict XVI katika mtandao wa Twitter.
Pichani juu ni Tweet za Papa Benedict XVI mpaka sasa.
PAPA Benedict wa 16 ametuma ujumbe wake wa kwanza kwenye akaunti yake yaTwitter. Ujumbe huu ulikuwa umesubiriwa kwa hamu sana.
Alionekana akibonyeza kwenye  iPad na kutuma ujumbe huo.
Ujumbe wake ulikuwa unasomeka hivi '' Marafiki wapendwa, nimefurahi sana kuwasiliana nanyi kupitia Twitter. Asanteni sana kwa ujumbe wenu na ninawabariki nyote kutoka rohoni.''
Msemaji wake alisema kuwa ujumbe wa Papa utamfikia kila mtu amjuaye kwa kutumia akaunti zake zilizo kwenye lugha saba.
Akaunti ya papa iliyo kwenye lugha ya kiingereza tayari ina wafuasi zaidi ya laki nane kwa sasa.
Akaunti zake zote ambazo ni @pontifex zinafuatana moja baada ya nyingine.
Mwaka jana Papa alituma ujumbe wake wa kwanza kutoka Vatican kuweza kuzindua mtandao wake wa maelezo mbalimbali.
Papa ni kiongozi wa waumuni bilioni 1.2 wa kikatoliki na atakuwa akitia saini ujumbe wake wala hatouandika mwenyewe.
Ujumbe wa papa kupitia Twitter unatarajiwa kuwajibu wafuasi wake kila wiki , kutoa baraka za Jumapili pamoja na kauli yake kuhusu matukio duniani.
Vatican imekuwa ikijaribu kutumia teknolojia za kisasa za mawasiliano kueneza imani, huku mwasisi wa Redio,
Guglielmo Marconi, akizindua redio ya kwanza ya Vatican mwaka 1931.
Kanisa Katoliki, pia tayari linatumia mitandao kadhaa ya kijamii ikiwemo YouTube, kuwasiliana na vijana.
Wasaidizi wa Papa wanasema kuwa papa mwenyewe, bado anapenda kuwasiliana na watu kwa maandishi kuliko kutumia kompyuta.
CHANZO: BBCSWAHILI,  PICHA NA : AFP/GETTY IMAGES

No comments:

Post a Comment