Friday, March 6, 2015

WAZIRI MAGUFULI KIBOKO, AAGIZA MKANDARASI APIGWE PINGU..KISA NI HIKI HAPA

Waziri wa ujenzi Dr John Pombe Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi na kukamatwa kwa aliyekuwa mhandisi mshauri wa jengo la ghorofa moja la ofisi ya mkuu wa wilaya ya Siha kwa kujengwa chini ya kiwango ili ajibu tuhuma zinazomkabili na kutoa wiki mbili kwa uongozi wa wakala wa nyumba (TBA) kukararabati jengo la ofisi ya mkuu wa wilaya ya Siha na mkuu wa wilaya ya Moshi ambayo yameonekana kutofaa kwa matumizi ya binadamu kutokana na kujengwa chini ya kiwango.
Waziri Magufuli ametoa agizo hilo baada ya kutoridhishwa na hatua zilizochukuliwa kushughulikia suala hilo baada ya kutembelea na kukagua jengo la ofisi ya mkuu wa wilaya ya Siha ambalo halifai kwa matumizi ya binadamu kutokana na kujengwa chini ya kiwango na kutoa maagizo kwa uongozi wa wabunifu na wakadiriaji majenzi pamoja na msajili wa wakandarasi.
 
Akitoa maelezo mbele ya waziri Magufuli afisa mtendaji mkuu wa wakala wa nyumba Elius Mwakalinga amemwambia waziri kuwa usanifu michoro ya jengo hilo ilikuwa sahihi lakini tatizo ni la mkandrasi ambe hakufuata vigezo vya ujenzi wa jengo hilo.
 
Katika tukio jingine akizungumza na wananchi wa Ngarenairobi waziri Magufuli amewahakikishia wananchi hao kuwa barabara ya kwa sadala kupitia sanya juu hadi Ngarenairobi itajengwa kwa kiwango cha lami baada ya waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Aggrey Mwanry kumwambia waziri magufuli adha wananchi ho wnayoipata ikiwa ni pamoja na kushindwa kusafirisha mazao yao pamoja kupanda kwa gharama za usafirishaji hususani nyakati za mvua.
 

Waziri Magufuli amehitimisha ziara yake mkoani Kilimanjaro ambapo akiwa njiani kurejea Dar es Salaam anatarajiwa pia kukagua ujenzi wa daraja la Kariakoo katika bonde la ruvu katika barabara ya Bagamoyo msata mkoani Pwani.

No comments:

Post a Comment