Sunday, May 3, 2015

FLOYD MAYWEATHER AMCHAPA MANNY PACQUIAO KWA POINTI


Floyd Mayweather akipozi na mikanda yake baada ya kumchapa Manny Pacquiao kwa pointi.
Mabondia hao wakitupiana masumbwi wakati wa mpambano huo.
Mayweather akimtupia makonde Pacquiao.
Pacquiao akimkabili Mayweather.
Nyomi iliyohudhuria pambano hilo la karne.
Floyd Mayweather wakati akielekea ulingoni.
Manny Pacquiao akiingia ulingoni.
Mayweather baada ya kumaliza mchezo.
Jamie Fox akiimba Wimbo wa Taifa wa Marekani.
Wimbo wa Taifa wa Ufilipino ukiimbwa.
BONDIA wa Marekani, Floyd Mayweather amemchapa mpinzani wake raia wa Ufilipino, Manny Pacquiao kwa pointi katika mpambano wao wa karne uliopigwa Ukumbi wa MGM Grand jijini Las Vegas leo asubuhi.
Majaji wa mpambano huo uliokuwa wa raundi 12 wamempa ushindi Mayweather kwa alama hizi: 118-110, 116-112, 116-112.
Baada ya pambano la leo, Mayweather ameshinda mapambano yake yote 48 aliyopigana hakiwa bado hajapoteza mchezo wowote.

No comments:

Post a Comment