Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania leo inaendeleza promosheni yake ya mji hadi mji "M-Pesa Tumewafikia" ukanda wa kaskazini mjini Same mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza na timu ya Mambo Jambo radio inayozunguka na wana Vodacom kanda ya kaskazini, mkuu wa msafara, Bw. Kahabi amesema promosheni ya "Tumewafikia" ni endelevu na inalenga kuwaelimisha wananchi kuhusu huduma ya malipo ya "M-Pesa" sambamba na kujishindia zawadi mbalimbali na punguzo maalum kwa simu za mkononi kutoka Vodacom.
Promosheni hio ilianza mji mdogo wa Hedaru na itaendelea, Same mjini, Moshi mjini, Usa river, Tengeru, Arusha mjini pamoja na Babati mjini.
Afisa Mwakilishi na Msimamizi wa Msafara, Bw. Abdallah amesema, "Wakazi wa Same mjini "Tumewafikia", lengo kuu ikiwa ni kuwaelimisha juu ya kujisajili M-Pesa, umuhimu wa kutunza namba za siri pamoja na viwango vya kutuma na kupokea fedha" hivyo fikeni kwa wingi leo tarehe 14/09/2012 saa nane na kuendelea katika promosheni yetu ya wazi eneo la stendi ya Same mjini ambapo bendi ya Mapacha Watatu itakuwa ikishusha burudani vilivyo".

No comments:
Post a Comment