Saturday, October 13, 2012

Atakayemfunika ROMA, Fid Q KUZAWADIWA GARI LA KIFAHARI


Fid QRoma Mkatoliki
KIJANA mkali atakayeonesha uwezo mkubwa kuwafunika wakali wa michano ya Hip-Hop Bongo, ROMA (pichani) na Fid Q kupitia Shindano la The Mic King lililoanzishwa jana na Ukumbi wa Dar Live, anatarajia kuzawadiwa mkoko wa maana kutoka kwa uongozi wa ukumbi huo, Erick Evarist anakupa mchongo kamili.
Kwa mujibu wa Mratibu wa Shindano hilo, Luqman Maloto, uzinduzi rasmi wa shindano hilo unatarajia kuanza kesho ndani ya kiwanja hicho cha kijanja cha Dar Live, pamoja na burudani zinazoendelea kudondoshwa kila Jumapili, mashabiki wa burudani watapata pia kushuhudia shindano hilo.
“Mchakato wa kuwasaka vijana wenye uwezo wa kuchana mistari umeanza tangu jana na unaendelea leo hivyo vijana ambao wanadhani wana uwezo, wazidi kujitokeza pale Dar Live ili kuratibiwa,” alisema Luqman na kuongeza:
“Niwasihi mashabiki wajitokeze kwa wingi kwani shindano ndiyo kwanza linaanza kuunguruma. Kesho ndiyo rasmi washiriki waliopenya kwenye uratibu wa awali, wataonesha uwezo wao jukwaani.”

No comments:

Post a Comment