Tuesday, January 1, 2013

PENTAGON ATANGAZA KUOA MKE WA TATU

Na Richard Bukos
MWANAMUZIKI tegemezi wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’ Ramadhan Mhoza ‘Pentagon’ ametangaza kuoa mke wa tatu aliyemtambulisha kwa jina la Pendo Mushi.
Mpango mzima ulipigwa chabo na paparazi wetu juzikati ndani ya Ukumbi wa Dar Live, ambapo wawili hao walionekana wakiwa katika pozi za kimahaba bila kuhofia macho ya wapambe nuksi.
Pentagon aliweka plain kuwa tayari ameshafanya mazungumzo na familia ya Pendo na kilichobakia ni mambo madogo ya kukamilisha ili wafunge ndoa na mrembo huyo kutoka pande za Kishumundu, Moshi mkoani Kilimanjaro.

No comments:

Post a Comment