MTANGAZAJI wa Channel Ten, Abdulkadir Nzige ameibiwa gari lake, Toyota Yarice lenye namba za usajili T527 BQV.
Ishu hiyo ilitokea Desemba 4, mwaka huu ambapo rafiki yake aitwaye Tamim Ramadhan alikwenda kumuazima gari lake ili akafanyie mizunguko yake ndipo alipotokomea nalo moja kwa moja.
Siku iliyofuata, Abdulkadir alimkuta rafiki yake huyo maeneo ya Ubungo, Riverside ambapo alijieleza kuwa ameibiwa gari maeneo ya Meeda baada ya kuwekewa madawa ya kulevya kwenye supu.
“Sikuridhika, nikampeleka polisi na kumfungulia mashtaka yaliyosomeka KMR/RB/14913/2012 WIZI WA GARI akashikiliwa na baadaye akatolewa kwa dhamana,” alisema Abdulkadir.
No comments:
Post a Comment