RAIS KIKWETE ZIARANI IGUNGA: AZINDUA UJENZI WA DARAJA LA MBUTU NA MRADI WA CHUJIO LA MAJI SAFI LEO
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia mashine ya kuchimbia mashimo ya nguzo za daraja na baadaye anakata utepe kuzindua ujenzi daraja la Mbutu la Igunga. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua mradi wa Chujio la maji safi kwa mji wa Igunga sehemu za Bulenya ambapo wakazi asilimia 70 wa mji huo watapata maji safi. Waziri wa Ujenzi, Dkt John Pombe Magufuli, akijiunga na bendi ya Msondo Ngoma kutumbuiza wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa daraja la Mbutu la Igunga leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na kutoa ushauri kwa kundi la vijana 10 ambao baada ya kumaliza chuo kikuu wamejikusanya na kuunda kikundi cha ujasiriamali mjini Igunga wakijishugulisha na Kilimo. Wananchi wakivuta katika sehemu itakayojengwa darala la kisasa la Mbutu la Igunga ambapo ujenzi wake umezinduliwa leo na Rais Jakaya Mrisho Kikwete, hatua ambayo itatatua kabisa tatizo la miundombinu. (PICHA NA IKULU)
No comments:
Post a Comment