Watani wa jadi Simba na Yanga leo wanakutana katika mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu Bara msimu huu. Katika mechi ya leo ambapo mwenyeji ni Simba SC itapigwa majira ya saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mechi ya mwisho kuwakutanisha watani hao ilikuwa ya msimu uliopita ambapo Yanga walishinda kwa bao 2-0. Kwa sasa Simba ina pointi 18 ikiwa kileleni wakati watani wao Yanga wana pointi 15 wakiwa nafasi ya nne.
No comments:
Post a Comment