Tuesday, October 22, 2013

ZA HIVI PUNDE: MAREHEMU JULIUS NYAISANGA KUAGWA MORO LEO NA DAR ES SALAAM KESHO


Marehemu Julius Nyaisanga (katiakati) enzi za uhai wake, kushoto ni meneja mkuu wa Global Publishers  Mrisho Abdallah na kulia ni Mhariri wa gazeti la Uwazi , Elvan Stambul.
Mbunge wa morogoro mjini na mmiliki wa abood Media Aziz Abood (Nyuma) akiingia nyumani kwa Marehemu Julius Nyaisanga Kihonda Viwandani Mjini Mororgoro.
Aliyekuwa mtangazaji maarufu wa redio nchini Tanzania, Julius Nyaisanga ambaye alifariki dunia jana katika hospitali ya Mazimbu Mjini Morogoro alipokuwa akipatiwa matibabu, anatarajiwa kuagwa leo mjini humo majira ya saa 11jioni nyumbani kwake Kihonda Viwandani baada ya kumaliza ibada ya kumuombea marehmu.
Baadaye mwili wa marehemu utasafirishwa leo majira ya saa 12 jioni kueleka jijini Dar es salaam ambako kesho wananachi wa jiji humo watapata fursa ya kuuaga mwili wa marehemu na kesho hiyo hiyo mwili wa marehemu utasafirishwa kwa ndege kwenda Tarime kwa mazishi.
Kabla ya kufikia maamuzi hayo wawakilishi kutoka wiraza ya habari na micheo na utamaduni pamoja na wajumbe kutoka l.T.V waliketi kikao na familia ya mrehemu na uongozi wa Abood Media na kukubaliana kwa pamoja kutoa fursa kwa wananachi ya Dar es salaama ambako Anko J ameishi na kufanya kazi kwa muda mrefu wapate pia fursa ya kuaga mwili wa marehemu.
NA DUSTAN SHEKIDELE,GPL MOROGORO NA MAKTABA/GPL

No comments:

Post a Comment