Thursday, August 9, 2012

DUDE APATA PIGO

 Dude Avamiwa na Majambazi......

 
Dude
Msanii maarufu wa filamu nchini Tanzania Kulwa Kikumba maarufu kama DUDE amevamiwa na majambazi usiku wa kuamkia leo tarehe 8/8/2012 kwake anapoishi Uwanja wa ndege jijini Dar es salaam....akiongea na thisisdiamond dude alisema kua yeye alikua yuko Kinyerezi katia harakati zake za kushuti movie usiku huo ambapo alimuacha mkewe na watoto wake watatu wakike wakiwa nyumbani usiku huo... alisema kua baada ya familia yake kula daku na kwenda kulala mida ya saa 9 usiku ndipo Majambazi hao waliingia na kupulizia sumu ndani ya nyumba hiyo ili waendelee kulala wasishtuke waanze kuiba... wezi hao walifanikiwa kuiba kila kitu ikiwemo Nguo,Muziki,Tv,Baloo la nguo la duka la dada yake kutoka china alilokua akiweka kwake kwaajili ya usalama na kadharika.... alisema wezi hao waliiba hadi vyakula vilivyobaki na gunia la mchele....asubuhi ya saa moja ndipo familia hiyo iliamka na kukuta kila sehemu kweupe watu wamekomba na milango yote iko wazi, ndipo bwana mkubwa wakampigia na kumpa taarifa hizo.

No comments:

Post a Comment