Mshambuliaji wa Malindi, Abdallah Abbas (kulia) akituliza mpira mbele ya mlinzi wa Duma, Mohamed Omar Mussa, wakati wa mchezo wa ligi kuu ya Grand Malt Zanzibar kwenye uwanja wa Amaan mjini Zanzibar jana. Malindi walishinda 2-0.
Mlinzi wa timu ya Duma, Mohamed Omar Mussa (kushoto) akipambana na mshambuliaji wa Malindi, Abdallah Abbas wakati wa mchezo huo.
Pambano la ligi kuu ya Grand Malt ya Zanzibar kati ya timu ya Malindi na Duma kwenye uwanja wa Amaan mjini Zanzibar jana lilimalizika kwa Malindi kuichabanga Duma mabao 2 - 0.
No comments:
Post a Comment