Wednesday, August 29, 2012

SIMBA SC

http://api.ning.com/files/L0l6eb69rSm*pAu0K5-eihSoiJqdIuiQ5JXQZgkV5IStDgetP05Iay3O7S1dLjZl-OmDZqdir8hIuyJNxyfPc1LKYYS4hdow/cico.JPG%3Fwidth%3D650
Kocha Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic.
Na Ezekiel kwa msaada wa Global Publishers.
KOCHA Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic, amesema idadi ya washambuliaji katika kikosi hicho, inampa ugumu wa kuamua nani acheze na nani asicheze.
Simba ipo jijini Arusha kwa zaidi ya wiki tatu sasa ikijiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara. Tayari Milovan ana ‘mashine’ saba zinazoweza kucheza kwenye safu ya ushambuliaji ambazo ni Felix Sunzu, Abdallah Juma, Daniel Akuffor, Kigi Makasi, Haruna Moshi, Mrisho Ngassa na Uhuru Selemani.
Milovan ameliambia gazeti hili kuwa, wachezaji hao wana viwango bora huku tofauti yao ikiwa ndogo, hali inayompa ugumu hasa katika mfumo anaotaka autumie, 4-3-3.
“Safu yangu ya ushambuliaji inanipa tabu katika kuamua nani aanze kwenye mechi kutokana na nyota wangu wote wanaocheza katika sehemu hiyo kuwa katika viwango bora.
“Tumecheza jana (Jumapili-dhidi ya Mathare United ya Kenya) tukatumia mfumo wa 4-3-3 lakini kila mchezaji aliyecheza katika sehemu ya ushambuliaji, ameonekana kuwa bora ingawa tofauti zipo lakini siyo kubwa sana, inapofikia hali kama hiyo kama kocha nafurahi lakini katika uamuzi inaniwia vigumu,” alisema Milovan.


No comments:

Post a Comment