Sunday, August 5, 2012

Simba yaleta straika kutoka Ivory Coast



KLABU ya Simba ipo katika hatua za mwisho za kumleta straika, Sihaone Abdulaziz, anayeichezea Stella Abidjan ya Ivory Coast.
Straika huyo anatarajiwa kutua nchini hivi karibuni kwa ajili ya kuichezea klabu hiyo katika msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa timu hiyo, Ismail Rage, alisema mshambuliaji huyo ataichezea Simba msimu mmoja kabla ya kwenda nchini Hispania kucheza soka la kulipwa.
Rage alisema ataichezea klabu hiyo kwa muda kutokana na mipango yake ya kwenda kucheza soka la kulipwa barani Ulaya.
“Ndani ya masaa 48 tutamtambulisha mshambuliaji mpya atakayesaidiana na Felix Sunzu, ambaye ni Sihaone Abdulaziz kutoka Ivory Coast.
“Mshambuliaji huyo atatuchezea kwa muda kati ya mwaka mmoja au miwili, kutokana na mipango yake ya kwenda kucheza soka nchini Hispania,” alisema Rage


Logo
Full nameSimba Sports Club
Nickname(s)Taifa Kubwa
Msimbazi Street Boys
Founded1936
GroundNational Stadium
Dar es SalaamTanzania
(Capacity: 60,000)
ChairmanIsmail Aden Rage
ManagerMilovan Cirkovic
LeagueTanzanian Premier League
2010-2011 league2nd
WebsiteClub home page

No comments:

Post a Comment