30 Septemba, 2012 - Saa 15:28 GMT
Wakaazi wa mji wenye bandari wa Kismayo, kusini mwa Somalia, wanasema bado mji huo haudhibitiwi na mtu yoyote.

Mizinga ilisikika usiku, lakini vikosi hivo bado viko nje ya mji.
Kuna taarifa kuwa wazee kadha wameuliwa na watu wenye silaha na shule na maduka karibu yote yamefungwa.
Kismayo ilikuwa ngome kubwa ya mwisho ya al-Shabaab, ambako wakiweza kuagiza silaha kutoka nchi za nje na kupokea pato kwa kuwatoza kodi wafanya-biashara.
No comments:
Post a Comment