Mwandishi wa habari wa mkoa wa Iringa wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi (pichani) ameuawa jioni ya leo katika kijiji cha Nyololo, wilayani Mufundi Iringa wakati wa vurugu zilizotokea baada ya wafuasi wa Chadema kuzuiliwa na jeshi la Polisi kufanya maandamano na mkutano usiokuwa na kibali. Mwangosi pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa habari wa Mkoa wa Iringa. Habari zaidi za tukio hili la kusikitisha zitajia kesho.
No comments:
Post a Comment