Ripoti iliyoandaliwa na BBC
imesema Serikali ya Kenya imekiri kwamba haiwezi kutimiza matakwa ya
walimu wa shule za misingi wanaogoma nchini humo huku mgomo huo ukiingia
siku ya pili.
Waziri wa elimu Mutula Kilonzo
amesema wanachotaka walimu yani kuongezwa asilimia miatatu ya mishahara
yao hakiwezekani, kwa sababu pesa hizo hazikujumuishwa kwenye makadirio
ya bajeti ya mwaka huu.
Maelfu ya walimu nchini Kenya
walianza mgomo wao jana (September 3) wakidai kuwa serikali imekuwa
ikipuuza kilio chao kuongezwa mishahara yao kwa miaka mingi ambapo
walimu hao ni wa shule za misingi na zile za upili.
Walimu hao wamekiuka agizo la
mahakama lililoharamisha mgomo huo huku shule nyingi katika miji mikubwa
kama Mombasa, Nairobi na Nakuru zilisalia kufungwa, walimu wa shule za
upili pamoja na wahadhiri wa vyuo vikuu wamesema watajiunga na mgomo huo
baadaee wiki hii ingawa tayari wameanza kususia kazi.
Mgomo huu umetokea wakati shule
zikifungua kwa muhula wa tatu kitu ambacho walimu hao wanasema sio hoja
kwani wamekuwa wakigoma kila muhula wa tatu unapofungua kwa zaidi ya
miaka kumi iliyopita wakidai hiyo nyongeza.
Wanasema kuwa serikali haina
usawa katika mishahara kwa wafanyakazi wa sekta ya umma kwani ni hivi
juzi tu wauguzi na wafanyakazi wengine wa umma waliongezwa mishara baada
ya kugoma lakini walimu wamepuuzwa.
Huu mgomo umeonekana kufanikiwa kwasababu hule nyingi zimesalia kuwa bila walimu na wanafunzi wengi wamebaki majumbani.
No comments:
Post a Comment