Na Mwandishi Wetu
KOCHA wa Simba, Milovan Cirkovic amesisitiza hata ugumu ukiwa vipi anataka kikosi cha JKT Ruvu ‘kiuwawe’ katika mechi ya Ligi Kuu Bara leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Simba ina pointi tatu kibindoni baada ya kushinda mechi yake ya ufunguzi wa ligi kwa kuirarua African Lyon kwa mabao 3-0 Jumamosi iliyopita.
Milovan aliliambia Championi Jumatano jana mchana kuwa, kabla ya mazoezi ya jana kila mchezaji alikuwa fiti kwa ajili ya mechi ya leo lakini hatamtumia mshambuliaji wake Felix Sunzu raia wa Zambia.
“Yoyote anaweza kucheza katika wachezaji isipokuwa Sunzu, nilizungumza naye baada ya kurejea amesema hakuwa akifanya mazoezi isipokuwa siku mbili tu alizokuwa hapa.
“Nampa muda wa kujifua zaidi, wengine wako fiti hadi mchana huu. Tunajua mechi itakuwa nguvu lakini matarajio yangu ni timu kucheza vizuri na kushinda,” alisema.
“Hatuna sababu ya kutofanya vizuri, hatuwezi kuidharau JKT ni kati ya wapinzani wakubwa na timu yenye mazoezi ya kutosha lakini ushindi ndicho ninachotaka.
Upande wa JKT iliyoanza ligi kwa kuifunga Ruvu Shooting kwa mabao 2-1, hadi jana walikuwa wanahaha kupata Uhamisho wa Kimataifa (ITC) wa Mussa Mgosi kutoka DR Congo alikokuwa akiichezea DC Motema Pembe. Kabla alikuwa mshambuliaji tegemeo wa Simba.
Hata hivyo bado JKT itamtumia mshambuliaji zamani wa Yanga, Omar Changa ambaye amekuwa akiisumbua sana Simba.

No comments:
Post a Comment