Na Wilbert Molandi
KOCHA Mkuu wa Yanga, Tom Saintfiet, amewaambia watani wake wa jadi kuwa anajua kwamba wamefurahia sare waliyoipata dhidi ya Tanzania Prisons, lakini amewasisitizia kuwa na wao watakiona cha moto watakapokwenda Mbeya.
Yanga ilitoka suluhu na Prisons katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Prisons, Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Akizungumza na gazeti hili, Saintfiet alisema mazingira ya Uwanja wa Sokoine ni magumu.
Amesema timu nyingine itakayokwenda kucheza huko ikiwemo Simba, itakiona cha moto, kwa kuwa Prisons wenyewe ndiyo waliozoea mazingira hayo.
Saintfiet alisema anawapongeza wachezaji wake kwa kucheza vizuri licha ya kukosa pointi tatu kutokana na mazingira ya uwanja.
“Najua wapinzani wetu Simba, wamefurahia sare tuliyoipata dhidi ya Prisons, lakini wakumbuke kuwa wenyewe nao wataenda kuuchezea Uwanja wa Sokoine na wataona kilichotupata sisi.
“Mashabiki wamekasirishwa na sare hiyo, lakini kikubwa kilichosababisha ni uwanja, nawaahidi kuwa mechi zijazo za ligi tutafanya vizuri na kuchukua ubingwa,” alisema Saintfiet, ambaye timu yake ilimaliza ligi iliyoisha ikiwa katika nafasi ya tatu chini ya kocha Mserbia, Kosta Papic.

No comments:
Post a Comment