Monday, September 17, 2012

UNAFAHAM KWAMBA WAKUVANGA WA ORIJINO KOMEDI ANAIMBA? SOMA ALICHOSEMA PIA SIKILIZA WIMBO WAKE MPYA HAPA.

Wakuvanga.
Tayari mpaka sasa wasanii wa kundi la vichekesho la ORIJINO KOMEDI TBC1 Mpoki, Joti na Masanja wanafanya muziki, kama hautambui naomba nikufahamishe kwamba Wakuvanga nae ameongezeka kwenye list ya wanaofanya muziki.
Amezungumza na millardayo.com na hapa namkariri aliyoyasema kwamba “mimi nafanya Komedi na ukiwa unafanya komedi una uwanja mpana unaweza kuwaigiza wanamuziki kwa hiyo nimetimiza vile vitu ambavyo vinahitajika kuwa comedian, nina sauti za Chidi Benz, Fid Q, Roma na wengine, sasa hivi sijatoa album nimeintroduce single inaitwa Angwisa, nilikua na sababu ya msingi ya kuifanya iwe ya kwanza kwenye album yangu, album na video viko tayari na vitasambazwa kuanzia tarehe 25 december 2012″
Kuhusu aina ya muziki alioufanya, Wakuvanga amesema “nimefanya Ragga, bolingo.. nyimbo nilizoimba zinafanana na wapagani, watu wa kanisa, ni nyimbo ambazo hazitukani, hazimtaji Yesu lakini inakidhi mahitaji ya watanzania”
Sentensi ya mwisho kutoka kwa Vengu ninayomkariri anasema “mimi nimewahi kujaribu vitu vingi kwenye maisha yangu, zamani tulikua tunajifunza kurap nilikua mchora katuni, nilijaribu vitu vingi nikajaribu na comedy na katika comedy ndio nimeweza kuwa comedian, sio mwanamuziki lakini muziki niliwahi kujaribu sikufanikiwa hii nafanya ni katika kutimiza ndoto zangu”

No comments:

Post a Comment