KILIMANJARO STARS YAIZAMISHA BAO 2-0 RWANDA, YATINGA NUSU FAINALI
KIKOSI cha Kilimanjaro Stras leo kimetinga hatua ya Nusu Fainali ya Michuano ya Chalenji inayoendelea nchini Uganda baada ya kuilaza bao 2-0 timu ya Rwanda 'Amavubi'. Bao la kwanza la Kili Stars limewekwa kimiani na Amri Kiemba dakika ya 33 ya mchezo baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Mwinyi Kazimoto wakati la pili likifungwa na mshambuliaji hatari, John Bocco dakika ya 54 ya mchezo akimalizia mpira uliotemwa na kipa wa Rwanda baada ya kushindwa kudaka shuti kali lililopigwa na Mwinyi Kazimoto. Kwa matokeo haya, Kili wanasubiri kucheza mchezo wa nusu fainali utakaopigwa siku ya Alhamisi Desemba 6 mwaka huu, wakati Amavubi wakiyaaga mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment