Sunday, September 16, 2012

WASANII WASHAURIWA KUJIHESHIMU ILI JAMII IWAHESHIMU PIA


Bob Junior

WASANII wameshauriwa kujiheshimu na kuwa na heshima juu ya kazi zao za sanaa ya muziki ili kufikia malengo waliyojiwekea katika maisha yao.

Tuhuma za kila siku kwenye baadhi ya vyombo vya habari haziwezi kumjenga msanii katika soko la muziki la kimataifa bali inachangia kumbomoa na kuvunja heshima yake kwa wadau na mashabiki wake wa muziki.

Wasanii wanatakiwa kuwa na uongozi utakaowaongoza na kuwapa mafunzo nini maana ya sanaa, msanii anatakiwa aweje na jinsi ya kutengeneza kazi zao ili waweze kufanya kazi ambazo zitakua na mvuto kwa jamii.

Kauli hiyo ilitolewa na mtayarishaji na msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Raheem Rummy ‘Bob Junior’ alipokuwa akielezea kuhusu uzinduzi wa staili yake mpya ya uimbaji inayoambtana na mwonekano wa mavazi pamoja na aina ya nywele.

Alisema kuwa mashabiki wake watarajie kumuona Bob Junior kuwa tofauti kuanzia mavazi mpaka uimbaji hii yote ni koboresha kazi zake ili zionekane zina ubora zaidi.

Aliongeza kuwa kwasababu anaheshimu kazi yake pamoja na kuwajali mashabiki wake hufikiria vitu vyenye ubora zaidi katika kazi zake.

No comments:

Post a Comment