Mecca Cheka warudi Arusha kutoka Nairobi, Kenya
Vijana wa kundi la Mecca Cheka, Rizy na Mwirora wakiwa katika pozi baada ya kurejea kutoka nchini Kenya.
Vijana Rizy na Mwirora wanaounda kundi la Mecca Cheka wamerudi kutoka Nairobi, Kenya baada ya kushiriki kikamilifu katika Pamoja Kids Concert iliofanyika Village Market Nairobi siku ya Jumapili tarehe 30 Septemba mwaka huu. "Tunamshukuru Mungu tulisafiri salama mpaka jiji la Kibaki mapokezi mazito toka kwa Sister Kakii ambaye ndiye mwenyeji wetu, mapumziko ya kutosha katika apartments tulizotengewa ready for makamuzi ya hatari for fans wetu wa Nairobi kesho yake. Tumejifunza mengi, muziki wetu unakubalika kuliko maelezo na Mecca cheka tumewakilisha vizuri pande za Kenya na shukrani tele ziende kwa mashabiki wetu all over Arusha kutusupport hadi kutambulika nchi jirani, Familia zetu, Producers wa ngoma zetu na Media house zote zinazosupport Mecca cheka movements.
No comments:
Post a Comment