Tuesday, October 2, 2012

RICK ROSS: ASKARI MAGEREZA ALIYEGEUKA BILIONEA


WAKATI habari ya mjini ikiwa ni ujio wa mkali William Leonard Roberts II ‘Rick Ross’ kunako Tamasha la Serengeti Fiesta Bongo, Oktoba 6, 2012, usilolijua kuhusu mkali huyu ni kwamba aliwahi kuwa askari magereza (Correctional Officer) kwenye Gereza la Florida kwenye miaka ya 1990 kabla ya kugeukia gemu la Hip Hop alikotusua mkwanja wa maana.
Sababu za mkali huyo kutema mzigo wa magereza hazijawekwa wazi ingawa inadaiwa kuwa tatuu alizojichora, rekodi ya makosa ya jinai kama matumizi ya bunduki, kukutwa na kitu cha marijuana na mengineyo, vilisababisha asimamishwe mzigo, akaona isiwe tabu, mwaka 2002 akaingia kwenye Rap Game na kuanza kuchana mistari na kugeuka bilionea.
Hip Hop imemlipa kinomanoma kwani mpaka sasa anamiliki mkwanja wa kutosha wa dola milioni 25 (zaidi ya Bilioni 37), mjengo wa maana pande za Miami, magari ya kisasa ya Maybach, Cardillac Escallade, Infinity QX56 na mengine kibao… si hivyo tu, mchizi pia anamiliki studio ya kisasa ya muziki ya Maybach Music, huku albamu yake mpya ya God Forgives, I Don’t ikikamata nafasi za juu kwenye chati kubwa duniani! Bhaas!

No comments:

Post a Comment