Siku kadhaa zilizopita shirikisho la soka nchini kupitia kamati yake ya ligi iliamua kumfungia mwamuzi mzoefu Mathew Akrama wa Mwanza aliyechezesha mechi namba 80 ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Simba iliyochezwa Oktoba 3 mwaka huu kwa madai ya kushindwa kuumudu mchezo huo wa watani jadi.
Kufungiwa kwa Akrama kulikuja baada ya
kelele zilizopigwa na vilabu vyote viwili pamoja wapenzi wake kwamba
mwamuzi huyo hakuchezesha kwa haki mchezo huo hivyo kuuharibu kabisa
kabisa mchezo wa kulwa na doto.
Sawa kwa amono yetu wapezni wa soka
tunaona Akrama weli aliboronga mchezo huo lakini kufungiwa kwake
kumekufanyika kwa utashi wa kisiasa kabisa kwa sababu ya usimba na
uyanga uliojaa kwenye soka letu.
Kisheria kamati ya ligi haikupaswa kukaa
kujadili suala la Mathew Akram kwa sababu hata FIFA inashauri na
kuagiza masula yote ya waamuzi na vyama vyao vyeme wataalam wa sheria za
soka, sidhani kama kwenye kamati ya ligi yumo mtalaamu yoyote wa
sheria.
Kama hayupo hii ni hatari hatari sana. FIFA inazuia watu wenye maslahi na vilabu kushughulika na masuala yoyote yanayohusu waamuzi kuanzia kupanga ratiba ya waamuzi mpaka kuwatolea maamuzi kama hili likiachwa likaendelea ni hatari katika maslahi ya mpira wetu kwa sababu waamuzi watachezesha kwa woga na kufikiria katika kamati kuna nani.
Mwamuzi anafundishwa siyo kufungiwa
au kuondolewa. Akikosea anaelekezwa makosa yake anapewa mchezo mwingine
ili kuona maendeleo yake na kama amerekebisha aliyoelekezwa.
Ndio maana hata kwenye ligi
zilizoendelea kama Uingereza marefa wakubwa kama akina Howard Webb muda
mwingine wanaboronga sana lakini ni mara ngapi tumewahi kusikia
wamefungiwa au wameondolewa kuchezesha ligi.
Kwanini? Kwa sababu inachukua Inachukua
takribani miaka kama 6 - 10
kumpata mwamuzi kama Akrama. Sasa wapo wangapi walioandaliwa kama yeye?
Hivyo badala ya kumuelekeza vizuri Akrama, refa ambaye ana uzoefu
tunaanza kuchukua marefa wachanga na mwishowe suala la kufungia waamuzi
halitoisha kwa sababu akikosea tu kwenye mechi ya watani atafungiwa na
kuletwa mwingine.
Vilevile inashauriwa kwamba katika mechi
kubwa kama ya Simba na Yanga makamisaa wanatakiwa kuwa marefa waastaafu
wenye uzoefu, sasa je katika mechi ya Simba na Yanga alikuwa mtu wa
aina hiyo? au alikuwepo tu mtu ambaye nae alikuwa tu ni refa wa kawaida?
Mwisho viongozi wa soka Tanzania tuache
kuuongoza mchezo huu kwa utashi wa kisiasa kwani hatotufanikiwa - kila
kitu kiende vile ambavyo kimepangwa na sio kufanya maamuzi kwa mazoea.
No comments:
Post a Comment