Dakika ya 4 ya kipindi cha kwanza: Amri Kiemba anaipatia Simba SC bao la kwanza baada ya kuunganisha pasi safi kutoka kwa Mwinyi Kazimoto. Simba 1, Yanga 0.
Dakika ya 28 ya kipindi cha kwanza: Mshambuliaji wa Simba, Edward Christopher anapewa kadi ya njano kwa kujiangusha ndani ya eneo la hatari.
Dakika ya 36 ya kipindi cha kwanza: Yanga wanafanya mabadiliko Hamis Kiiza anakwenda benchi anaingia Frank Domayo.
Dakika ya 44 ya kipindi cha kwanza: Beki wa Yanga Mbuyu Twite anazawadiwa kadi ya njano
Half Time: Simba 1, Yanga 0.
Dakika ya 46 kipindi cha 2: Kavumbagu anaingia kuchukua nafasi ya Nizar Khalfan
Dakika ya 64 kipindi cha 2: Said Bahanuzi anaipatia bao la kwanza Yanga kwa penati baada ya beki wa Simba, Paul Ngalema kuunawa mpira ndani ya penati box.
Dakika ya 66 kipindi cha 2: Daniel Akuffo anaingia kuchukua nafasi ya Edward Christopher.
Dakika ya 70 kipindi cha 2: Haruna Moshi wa Simba anaingia kuchukua nafasi ya Jonas Mkude.
Dakika ya 79 kipindi cha 2: Simon Msuva anapewa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya beki wa Simba Juma Nyosso.
Dakika ya 82 kipindi cha 2: Beki wa Yanga, Kelvin Yondani anatolewa uwanjani baada ya kuumia na nafasi yake inachukuliwa na Juma Abdul.
Dakika ya 88 kipindi cha 2: Mwinyi Kazimoto anaumizwa na nafasi yake inachukuliwa na Ramadhan Chombo 'Redondo'.
MECHI IMEKWISHA. MATOKEO SIMBA 1, YANGA 1.
No comments:
Post a Comment