MCHUJE RAFIKI
Una rafiki wa jinsi tofauti. Mwenzi wako ameambiwa kwamba wewe una uhusiano naye wa kimapenzi. Unachotakiwa kufanya ni kugundua kwamba huyo rafiki yako anamsababishia mateso mwandani wako. Jaribio la kwanza ni kuhakikisha unamtoa hofu mpenzi wako.
Ikitokea umejaribu kufanya hivyo lakini bado mpenzi wako hana imani na huyo rafiki, haraka sana ‘mdiliti’. Tambua kwamba amani ya mpenzi wako inajenga mara 100 usalama wako. Uking’ang’ania kotekote, utapata shida mno mbele ya safari.
Wakati mwingine hutokea mwenzi wako anakuwa na wivu wa kupitiliza. Hata ukimwambia vipi hataelewa uhusiano wako wa kirafiki na mtu wa jinsi tofauti. Basi cha kufanya ni kupima faida. Inawezekana pia mpenzi wako mwenye wivu ndiye kirusi.
Sasa basi, kwa maslahi ya maisha yako ya leo na kesho, unatakiwa kufanya uamuzi sahihi. Je, kuendelea kumuendekeza mpenzi wako mwenye wivu au kuachana na rafiki anayemsababishia mateso mwandani wako? Ukichekecha na kupima vizuri, utajua uamuzi sahihi ni upi.
Pengine huyo rafiki ni mshirika wako kikazi au kibiashara. Tangu umeanza kushirikiana naye, kuna unafuu mkubwa wa kimaisha na hatua kubwa umepiga. Hapo sasa jukumu ni lako, kusuka au kunyoa. Palipo na hasara, hakikisha unadhibiti. Mapenzi hayapaswi kugeuka nyundo ya kukurudisha nyuma kimaisha.
KABILIANA NA WIVU
Kila mtu anatakiwa awe na wivu ili mambo yaende sawasawa. Itashangaza sana pale utakapoambiwa mpenzi wako anasaliti na umethibitisha halafu ukaendelea kuwa na tabasamu lilelile. Kukosa wivu maana yake una kasoro za kibinadamu. Inatakiwa uchunguzwe.
Hata hivyo, wivu ukizidi hasa ule wenye kuibua matatizo ni hatari mno. Kisa wivu ndiyo umfanye mwenzi wako ashindwe kutimiza majukumu yake ya kila siku? Hutaki awasiliane na watu, unaonesha wivu mpaka unaonekana kiherehere? Wewe ni kirusi, nashauri udilitiwe.
Mapenzi bora ni yale yanayokwenda sambamba na ujenzi bora wa kimaisha. Haiwezekani tangu mmeanzisha uhusiano, uchumi unazidi kuporomoka. Inapotokea hali ya aina hiyo, ujue kuna kasoro kubwa ndani yenu. Wewe au yeye, mmoja ni tatizo. Usikubali kufeli kimaisha kisa mapenzi.
Mizunguko yako ya kikazi, inakutaka ukaribiane na watu mbalimbali bila kujali jinsi zao. Mwenzi wako haelewi kuhusu hilo, matokeo yake anakuwa kikwazo kikubwa kwenye utendaji wako. Ukipigiwa simu ya kazi, yeye anawaza ni mapenzi. Anakuharibia.
Kwa faida ya maisha yako unatakiwa kumwepuka mapema mpenzi anayekuonea wivu mpaka anakwamisha shughuli zako. Mpenzi bora ni yule anayekupa wepesi wa kutimiza majukumu yako ya kila siku. Haiwezekani akawa anakudidimiza.
HUPASWI KULIA, TAFAKARI JINSI YA KUAMUA
Hapa naona ni busara kwanza kufafanua kuwa wakati mwingine Mungu anataka tukutane na watu ambao sio sahihi kwanza ili tukikutana wa watu sahihi, tujue jinsi ya kuwatunza, kuwathamini na kujivuna kuwa nao.
Unaweza kuwa na mwenzi bora lakini usigundue, ukamfanyia vitimbi. Wengine hutambua kwamba mume au mke wake alikuwa bora mpaka pale watakapoachana. Hivyo basi, ukishayaona kwa mtu ambaye siyo sahihi, siku ukimpata anayekidhi matakwa ya moyo wako, lazima utajivunia zawadi uliyopewa na Mungu.
Mara nyingi hutokea unakutana na mtu ambaye anamaanisha mno kwako lakini kutokana na historia yako ya kuumizwa huko nyuma, ukawa humuamini, kwa hiyo ukamuacha na yeye aende. Hupaswi kuwa na uamuzi wa jazba kwenye mapenzi. Tafakari, fanya uchunguzi halafu uitafakari kwa kina ripoti ya uchunguzi wako kabla ya kuamua.
Itaendelea wiki ijayo, Jumamosi.

No comments:
Post a Comment