WANACHAMA wa
Chama cha Mapinduzi (CCM) wa Vijiji vinne vya Kata ya Sungaji Mvomero,
wanadaiwa kuomba kuhamia Chama cha CHADEMA wakisema wameudhiwa na hatua
zilizochukuliwa na Serikali na CCM kushughulikia Mgogoro wa Mapigano ya
Wakulima na Wafugaji.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili jana zinadai, hayo yamesemwa wakati wakichagishana fedha kwa ajili ya kuwaweka Mawakili watakaowatetea ndugu zao wanaokabiliwa na kesi ya Mgogoro wa Mapigano ya Wafugaji na Wakulima yaliyokomeshwa hivi karibuni baada ya kusababisha Maafa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya wana CCM hao wa Mkindo, Hembeti, Mbogo na Kigugu walioomba wasitajwe majina walisema, mara watakapomaliza kukusanywa fedha kwa ajili ya kuwawekea Dhamana na Mawakili ndugu zao, watatangaza rasmi kukihama CCM na kuhamia Chadema.
“Kuna ndugu zetu, wanafunzi wasio na hatia wamekamatwa na kuwekwa ndani wakihusishwa na Vurugu za Mapigano ya wakulima na Wafugaji, wakati hawakuwepo eneo la mapigano, wakati wanawaacha waliohusika na kusababisha maafa hayo.
Watoto wetu sasa wanakosa masomo, hawasomi, wanapata adha wasiyoistahili. Je watasoma lini wakati wanashinda Lupango?”. alilalamika Mama mmoja aliyeomba asitajwe jina lake lakini baadaye ilibainika ni ndugu wa Kiongozi mmoja wa CCM wa Mbogo aliyeko ndani.
Uchunguzi uliofanyika vijijini humo imebainika tayari zimeshachangwa zaidi ya Sh. Laki Tatu kila kijiji ili zitumike kwa ajili ya kuwawekea dhamana na Mawakili watuhumiwa hao, ambao baadhi yao ni viongozi wa CCM katika vijiji hivyo.
Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Sungaji, Mussa Kombo, alipoulizwa iwapo ni kweli wana CCM hao wa vijiji vinne wamepeleka Maombi ya kukusudia kujiunga na Chama chake alisema,
“Mimi nilikuwa Safari kwenye Msiba wa Kaka yangu Magubike, aliyeuawa na watu wasiojulikana na kunyang’anywa Ng’ombe 60. Nimesikia taarifa za namna hiyo, hivyo uwe na subira tutakujulisha wewe na wandishi wenzio”.alisema Kombo.

Chadema yamjibu Nape
Mnyika kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari alisema Chadema tangu kuanzishwa kwake kimekuwa kikiheshimu katiba yake kwa kufanya chaguzi zake kwa mujibu wa katiba, kanuni, maadili, itifaki ya chama.
“Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita alichokizungumza Nape, Chadema kimefanya chaguzi mara mbili kila baada ya miaka mitano kama katiba na kanuni zinavyohitaji,”alisema Mnyika.
Alisema Chadema kimefanya uchaguzi mkuu wa ndani mwaka 2004 na kikafanya uchaguzi mkuu mwingine mwaka 2009 mara baada ya kipindi cha miaka mitano ambayo ni muda wa kawaida wa uongozi.

No comments:
Post a Comment