

“Nimeupenda uteuzi wa waigizaji wa Siri, na najua watazamaji watawapenda pia,” alisema kwenye mahojiano.
Mwanzoni mwongozaji huyu kijana alitaka kukata tamaa alipoona mzigo huu ni mkubwa. Jukumu lake la kwanza lilikuwa kuchagua waigizaji kati ya wasanii 2000, wengi wazoefu, lakini wengi wengine wapya, kwa ajili ya tamthilia iliyopambwa na visa vikali vinavyogusa ndani kabisa maisha ya watu.
“Kulikuwa na vitu vingi vya kufanyia kazi. Lakini niligundua mchanganyiko madhubuti wa visa na vichekesho ndani ya hadithi uliofurahisha sana. Tunashughulika na masuala mazito, yanayogusa sana maisha ya watu, lakini tunayafanya katika njia ya kuchekesha ambayo watu wataburudika.”
Uzuri wa filamu, anaelezea Riber, ni kwamba inawaruhusu watazamaji kuamka na kuwa “karibu na wahusika wetu”.
“Tunaweza kuingia ndani ya mawazo yao na kuwa sehemu ya hisia zao za ndani. Tunaweza kuwa sehemu ya nini kinachowatesa na yapi yanayowafanya wapende na kuchukia.”
Asilimia 40 ya tamthilia hii ilipigwa studio na asilimia 60 ilipigwa sehemu nyingine, zikichukua wiki tatu Bagamoyo, kilomita hamsini kaskazini mwa Da res Salaam. Riber anasema watendaji walipokewa vyema na watu na viongozi wa Bagamoyo, na kwa kweli ilikuwa ni starehe kupigia picha katika eneo zuri kama lile.”
Tathmilia hii itaonyeshwa saa 3:30 usiku kila Jumapili kwenye ITV, na saa 3:30 usiku kila Jumatano kwenye EATV!
No comments:
Post a Comment