--
Vodacom yazindua duka jipya la mauzo barabara ya Samora.
- Duka hilo linatarajia kupunguza msongamano wa wateja kwenye maduka mengine.
- Idadi ya maduka ya Vodacom jijini yafikia 6.
Dar es Salaam, Vodacom Tanzania imeongeza duka lake lingine na kufikisha idadi ya maduka sita katika jiji la Dar es Salaam, ambapo duka hilo linatarajiwa kukidhi ongezeko la mahitaji ya huduma kwa wateja.
Duka hilo jipya lililoko barabara ya Samora, eneo la Posta, Dar es Salaam, linatarajia kupunguza msongano wa wateja katika maduka yaliyopo sasa, likiwemo duka la Mlimani City, Mtaa wa Ohio, RDK Victoria na Barabara ya Ali Hassan Mwinyi.
Baadhi ya huduma zitakazotolewa katika duka hilo ni pamoja na kuunganishwa na huduma za Intaneti, mauzo ya muda wa maongezi, mauzo ya bidhaa na kuunganishwa na huduma mbalimbali, pamoja na kusajili kadi za simu, huduma ya M pesa na nyinginezo.
Duka hili litafunguliwa kila siku za Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni, na Jumamosi saa 3 asubuhi hadi saa 7 mchana. Jumapili na siku za sikukuu hakutakuwa na huduma.
Ofisa Mkuu wa Mauzo na usambazaji wa Vodacom Tanzania Hassan Saleh, amesema anatarajia kuwa duka hilo jipya litakidhi mahitaji ya ongezeko kubwa la wateja wa Vodacom hasa katika jiji la Dar es Salaam.
“Tunajivunia kufungua duka hili, kwani tumetengeneza ajira kwa wafanyakazi wapya. Hadi kufikia sasa, Vodacom imetoa ajira za moja kwa moja kwa wafanyakazi 500 na wengine zaidi ya 30,000 wenye ajira zisizo za moja kwa moja,” anasema Saleh.
Kwa duka hili jipya, anasema Saleh, Vodacom itaendelea na azma yake ya kutoa huduma bora kwa wateja wake. “Tumewekeza kwa kiasi kikubwa katika kuboresha mtandao wetu na kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma zenye ubora wa hali ya juu na za kisasa, kupiga simu na kutuma SMS na huduma za Intanet,” alihitimisha Saleh.
---
Kuhusu Vodacom Tanzania:
Kampuni ya Vodacom Tanzania Limited ina dhamira ya dhati ya kushirikiana na jamii katika shughuli za maendeleo kupitia taasisi yake ya Vodacom Foundation. Vodacom Foundation ina nguzo kuu tatu: Afya, Elimu na Ustawi wa Jamii. Hadi sasa taasisi hiyo imechangia zaidi ya miradi 120 ya kijamii nchini. Aidha, imeshinda tuzo mbalimbali za kitaifa na za kimataifa katika nyanja ya Uwajibikaji wa Mashirika kwa Jamii. Hizi ni pamoja na East African CSR Awards na Diversion and Inclusion Award ambayo hutolewa na kampuni mama ya Vodafone .
Vodacom Tanzania Limited ni kampuni ya simu za mikononi inayoongoza Tanzania inayotumia teknolojia ya kisasa ya mawasiliano. Vodacom Tanzania ni kampuni tanzu ya Vodacom Group (Pty) Limited, South Afritca, ambayo pia ni kampuni tanzu ya Vodafone Group UK. Vodacom Group (Pty) Limited inamiliki hisa ailimia 65 Vodacom Tanzania na asilimia 35 zilizobaki zinammilikiwa na Mirambo Ltd.
Vodacom Tanzania imetangazwa kuwa Super Brand (Chapa Bora Zaidi) kwa miaka mitatu mfululizo, kutoka 2009 -2011.
Kwa mawasiliano:
Matina G. Nkurlu
Meneja Mahusiano
Vodacom Tanzania Limited.
Mlimani City Jengo namba 1. Ghorofa ya kwanza.
Simu namba: 0754 710 099
Email:mnkurlu@vodacom.co.tz
Kwa taarifa zaidi kuhusu kazi za Vodafone Foundation, Tembelea.
No comments:
Post a Comment