
Viongozi wa Tawi la Chadema DMV wakiwa katika sherehe ya kuuaga mwaka 2012 na kukaribisha mwaka mpya 2013, Siku ya Jumamosi katika ukimbi wa Mirage Hall uliopo maeneo ya Hyattsville Maryland nchini Marekani.

Mwenyekiti wa Chadema Tawi la DMV, Mhe. Cosmas Wamura, akiwahamasisha wana DMV kuhusu mipangilio ya Chama pamoja na kusisitiza mpango mzima wa kujiunga na tawi hilo liliopo Washington DC kwa nia njema ya kuitakia Tanzania mabadiliko ya M4C katika mwaka mpya wa 2013 ambao ni mategemeo makubwa ya kusonga mbele.

Katibu mwenyekiti wa wanawake, Mhe. Baby Mgaza wakati akizungumza na wana DMV katika mkutano huo uliofanyika Siku ya Jumamosi Desemba 22, 2012 ndani ya ukumbi wa Mirage.

Wana DMV waliohudhuria katika hafla hiyo wakipata flashi ya pamoja katika sherehe ya kuaga Mwaka 2012 na kukaribisha mwaka mpya 2013 M4C.

Baadhi ya Makada wa CCM DMV, Katibu Mwenezi Benjamin Mwaipaja (wa pili kushoto) akiwa na Yasini Landi wa kwanza kulia, kama kawaida yao wakisherehekea kama Watanzania wanaojali taifa lao!

Aliyekuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Tawi la Chadema, Bw. Kaley Pandukizi akiwahamasisha wana DMV katika mpango mzima wa kuaga Mwaka 2012 na kukaribisha mwaka mpya 2013 M4C.

Katibu wa Chadema DMV, Mhe. Isdori Focus Lamuya akitoa changamoto za kukitakia chama chake maendeleo na ushirikiano mwema katika mpango mzima wa kuaga Mwaka 2012 na kukaribisha mwaka mpya 2013 M4C wakati alipokuwa akizungumza na wana DMV kwenya mkutano huo uliofanyika Siku ya Jumamosi Desemba 22, 2012 ndani ya ukumbi wa Mirage.

Wanachama wa Chadema DMV wakiwa pamoja na baadhi ya wana DMV katika sherehe hiyo.
KWA PICHA ZAIDI TEMBELEA swahilivilla.blogspot.com
No comments:
Post a Comment