Monday, December 24, 2012

PATAWAKA MOTO ‘VODACOM DAR LIVE’ SIKUKUU YA X-MAS

Usiku wa Krismas ‘Vodacom Dar Live’ kupambwa na Diamond, Dimpoz
Dar es Salaam, Desemba 24, 2012.
Msanii wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’ amepania kudhihirisha umwamba wake dhidi ya msanii mwenzake Ommy Dimpoz, katika shoo yao ya pamoja inayotarajiwa kufanyika sikukuu ya Krismas, kwenye ukumbi wa Vodacom Dar Live.
Diamond  ambaye mara kadhaa amekuwa akitamba kuwa na utajiri wa mashabiki ndani na nje ya nchi amesisitiza kuwa katika tamasha hilo atamfundisha Dimpoz namna muziki unavyopaswa kuwa.
“Nawaomba mashabiki wangu mfike kwa wingi, nawahakikishia Dimpoz haniwezi kwenye gemu, nataka nimfundishe namna ya kuitumikia tasnia hii,” anatamba Diamond katika mazungumzo yake wakati wa hafla ya utambulisho wa usiku wa Diamond & Dimpoz uliofanyika Dar es Salaam juzi.
Kwa upande wake Dimpoz amesema yeye si mtu wa Maneno mengi, nazaidi amemtaka swahiba wake ajiandae na shoo hiyo, na mashabiki ndio watakaoamua juu ya tambo zilizopo.
Aidha katika mkesha huo kutakuwa na burudani kadhaa zitakazo poromoshwa ambapo Bendi ya Extra Bongo na msanii mkongwe Juma Nature ni miongoni mwa wasanii watakaopagawisha.
Pamoja na burudani hizo, mchana kutakuwa na pambano la masumbwi kati ya Mbwana Matumla na David Charanga kutoka Kenya.
Kabla ya pambano hilo, bondia Mada Maugo atavaana na Yiga  Juma wa Uganda, na Bahati Mwafyela atachapana na Chupaki Chipindi.

No comments:

Post a Comment