Monday, February 11, 2013

CCM YAENDESHA SEMINA YA MIKAKATI YA KUONDOA TATIZO LA AJIRA NCHINI



Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa akibadilishana mawazo na Waziri wa Kazi na Ajira Mheshimiwa Gaudencia Kabaka wakati wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM ambapo leo semina ilikuwa juu ya Mikakati ya Kuondoa tatizo la ajira nchini.
Katibu wa NEC,Uchumi na Fedha, Zakia Meghji,akibadilisha mawazo na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi pamoja na Katibu Mkuu  Ndugu Abdurahaman Kinana  leo, Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Ndugu Mwigulu Nchemba  akijadiliana jambo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa wakati wa semina juu ya kuondoa tatizo la ajira nchini.
Katibu wa NEC ,Itikadi na Uenezi na Katibu wa NEC,Uchumi na Fedha wakijadili jambo la ajira kwa nchi nzima wakati wa semina ya mikakati ya kuondoa tatizo la ajira nchini, leo kwenye ukumbi wa NEC, Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wakifuatilia kwa makini semina juu ya Mikakati ya kuondoa tatizo la ajira nchini.

No comments:

Post a Comment