Wednesday, February 13, 2013

DHAIRA FITI KUIVAA LIBOLO, MAFTAH, NYOSSO NDANI

Na Khadija Mngwai
KIPA wa Simba, Abel Dhaira, yupo fiti kuivaa Recreativo do Libolo ya Angola katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika unaotarajiwa kuchezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Dhaira, raia wa Uganda, hakuwahi kuidakia Simba tangu aliposajiliwa katika mzunguko huu wa pili kufuatia kuwa majeruhi wa nyama za paja alizoumia akiwa Oman timu hiyo ilipokwenda kuweka kambi ya wiki mbili.
Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema Dhaira kwa sasa yupo fiti kucheza mchezo huo kutokana na kupona majeraha yake.
kuichezea timu ya taifa, kwa sasa yupo fiti kuivaa Libolo, hivyo utabaki uamuzi wa kocha Liewig kuamua ampange nani katika mechi hiyo kati yake na (Juma) Kaseja.
“Wachezaji wengine ambao nao wanatarajiwa kujiunga na wenzao katika mchezo huo ni pamoja na Amir Maftah, Juma Nyosso na Haruna Moshi ‘Boban’ baada ya kumalizana na uongozi.
“Mashabiki watarajie mambo makubwa zaidi katika mchezo huo, kwani tumeimarisha kikosi kwa kuhakikisha lazima tunashinda katika mchezo wa nyumbani kwa kuwa Simba inayocheza katika ligi itakuwa tofauti na ile inayocheza mechi za kimataifa,” alisema Kamwaga.
Alimalizia kwa kusema,uongozi wa Simba umeamua kumuongeza kocha Talib Hilal katika benchi la ufundi ili kuweza kuongeza nguvu na kuhakikisha wanafanya vizuri.

No comments:

Post a Comment