Saturday, September 21, 2013

KINANA AJILIPUA BUNDA,HAYUKO TAYARI KUONA WATENDAJI WA SERIKALI WANAIANGUSHA (CCM)‏


1
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Busega Ndugu Paul Mzindakaya.
5
Kinana akisalimiana na wabunge deo Filikunjombe wa jimbo la Ludewa na Kangi Lugora wa jimbo la Mwibara. 6
Kinana akisalimiana na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi mara baada ya kuwasili Sereneti leo.
10
Kinana akicheza na wananchi waliokuwa wakiimba nyimbo za kumkaribisha katika kijiji cha Namibu katika jimbo la Mwibara.
8
Kinana akilakiwa na Mbunge wa jimbo la Mwibara Kangi Lugora mara baada ya kuwasili katika jimbo la Mwibara.
7
Kinana akizungumza na Mh Waziri Steven Wasira wakati alipotembelea mradi wa maji katika kijiji cha Nyabeho wilayani Bunda.
6
Kinana akisalimiana na watendaji wa chama hicho mkoani Mara.10
Kinana akifurahia ngoma wakati alipowasili katika kijiji cha Nabiru jimbo la Mwibara.11
Hili ndiyo jengo linalojengwa la Chuo Cha Veta huko Mwibara.13
Kinana akishiriki kujenga jengo hilo la Veta Mwibara mkoani Mara.
14
Kinana na Ndugu Nape Nnauye katibu wa Itikadi Siasa na Uenezi wakinawa mikono baada ya kushiriki katika maendeleo ya elimu.
27
Umati wa wananchi waliohudhuria kwenye mkutano huo uliofanyika Stendi mjini Bunda.
28
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akiwahutubia wananchi mjini Bunda
29
Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na wananchi wa jimbo la Bunda leo.
30
Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Bunda leo.
20
Kinana akinong'onezana jambo Mbunge wa jimbo la Ludewa .
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana, amewasili Wilaya ya Serengeti kata ya Nzugu Mkoani Mara akitokea Wilaya Busega Mkoa mpya wa Simiyu na kuanza ziara ya siku 6 katika mkoa wa Mara akianzia Wilaya ya Bunda mkoani humo, Kinana amekagua miradi mbalimbali katika jimbo la Mwibara na Bunda na kufanya mkutano wa hadhara mjini Bunda akikemea watendaji wa serikali ambao hawataki kuwajibika badala yake wamekalia kuvaa suti, kung'ang'ania vikao huku kujilipa posho na kuwa "Mamangimeza" badala ya kuwatumikia wananchi jambo ambalo Chama cha Mapinduzi ambacho ndiyo kimeiweka serikali madarakani hakitakubali badala yake kitawawajibisha watendaji hao kukinusuru chama cha Mapinduzi, Kinana amesema yuko tayari kujilipua ili kutetea wananchi na Chama cha Mapinduzi CCM ili kurudisha heshima ya chama kama Mwalimu alivyokiacha.
PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-BUNDA

No comments:

Post a Comment