Ili kutambua na kuthamini mchango wa wanawake katika maendeleo ya jamii na taifa kwa jumla, Kampuni ya Global Publishers and General Enterprises Limited, inatoa tuzo kwa mwanamke ambaye katika maisha yake amefanya mambo mengi zaidi ambayo yamenufaisha na kuboresha maisha ya watu.
Mchakato wa kumsaka na kumtunuku mwanamke huyo umepewa jina la 'Women of The Year Award' ambapo kasi ya upigaji kura kwa sasa ni kubwa kwani zimeanza kumiminika.
Washiriki watano wanaowania nafasi hiyo, wasifu wao kwa ufupi na video zao ni kama ifuatavyo:

DK. MARIA KAMM (MK)
Ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Mama Clementina inayoendesha shule ya wasichana wanaotoka kwenye mazingira magumu nchini ambao wanaandaliwa kuwa wajasiriamali na viongozi bora katika jamii. Amezaliwa mwaka 1937 mkoani Iringa. Ni mama, mwalimu, mwanasiasa, mfanyabiashara, mtetezi wa haki za binadamu anayeng’ara katika historia ya wanawake wa Tanzania. Aliwahi kuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Weruweru ya mkoani Kilimanjaro kwa miaka 22, kuanzia mwaka 1970 hadi 1992.

Akiwa mkuu wa shule hiyo alifanikiwa kuzalisha wasichana ambao wengi wao kwa sasa ni viongozi wenye majukumu makubwa kijamii.
Kati yao ni pamoja na Dk. Asha-Rose Migiro, Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Dk. Mwele Malecela, Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Helen Kijo-Bisimba, aliyekuwa Balozi wa Tanzania Marekani, Mwanaid Maajar na wengineo wengi.
Pia aliwahi kuwa mbunge katika Bunge la kwanza la Tanganyika na mbunge wa Viti Maalum (CCM) kuanzia mwaka 1990 hadi 2000.
Amekuwa akiishauri serikali kuhusu suala la wasichana wanaopata mimba wakiwa shuleni waweze kurejea kuendelea na masomo baada ya kujifungua ili wapate elimu ya kuwasaidia kulea watoto kuliko kuwafukuza moja kwa moja shuleni na kuzima ndoto zao kabisa. Pia amekuwa akitoa miongozo kwa serikali kuhusu kuboresha elimu na kurejesha baadhi ya masomo ili kuhakikisha shule zinamiliki miradi yake.

MSIKILIZE DK. MARIA KAMM HAPA:

Hadi kuteuliwa kwa cheo cha Umoja wa Mataifa alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Januari 2006.
Chini ya Rais Benjamin Mkapa, alikuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto pia alikuwa mbunge kupitia viti maalumu kwa wanawake.
Kabla ya kujiunga na siasa alifundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Ana shahada ya uzamili ambapo mwaka 1992 akaongeza cheti cha udaktari wa sheria kwenye Chuo Kikuu cha Konstanz (Ujerumani). Kabla ya kurejea Tanzania kufundisha. Ameolewa na Cleophas Migiro na wana watoto wawili wa kike.
Kwa sasa ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.
KUMSIKILIZA DK. ASHA–ROSE MIGIRO BONYEZA VIDEO HAPA CHINI:

Amezaliwa Januari 9, 1956. Ni mbunge wa kuchaguliwa wa Jimbo la Same-Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi. Aliwahi kuwa Mhasibu wa KLM Airline, Mhasibu Msaidizi wa Air Tanzania Corporation (ATC) na Mdhibiti Fedha wa Gulf Air Corporation.
Pia aliwahi kuwa mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Kisutu na Mwenyekiti wa UWT, Wilaya ya Kinondoni. Amekuwa kinara wa kupiga vita ufisadi kwa kuwasema mafisadi waziwazi na kusababisha waache uporaji wa rasilimali za Watanzania.
Ni mke wa mwanasiasa mkongwe nchini, Mzee John Malecela.
MSIKILIZE ANNA KILANGO MALECELA HAPA CHINI:

Huyu ni mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini mkoani Kagera kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Amezaliwa Oktoba 12, 1950 huko Kagabiro wilayani Muleba, Mkoa wa Kagera. Ni msomi wa kiwango cha uprofesa. Wanawake maprofesa nchini ni wa kuhesabu. Aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa (UN-HABITAT) kuanzia Machi 2006 hadi Novemba 2010. Ana watoto wanne.
MSIKILIZE PROF. ANNA TIBAIJUKA HAPA:

Huyu ni mama jasiri, amejitokeza kupigania haki na usawa wa wanawake na watoto. Amepambana kukomesha ukeketaji, mimba za utotoni, ukatili wa kijinsia na hasa kuhakikisha vyombo vya habari vinaandika na kufichua madhambi yote ya kuwanyanyasa na kuwatesa wanawake na watoto.
Mama Ananilea Nkya, alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) tangia 2001 hadi mwaka huu alipomaliza kipindi chake.
Mama huyu alianza kazi ya uandishi wa habari 1982 RadioTanzania na wakati anajiunga na TAMWA 2001, alikuwa amepanda hadi naibu mhariri ndani ya Redio Tanzania na kuendesha kipindi cha kutetea haki za wanawake –MWANGAZA.
KUMSIKILIZA ANNANILEA NKYA BONYEZA VIDEO HAPA CHINI:
KUMPIGIA KURA MWANAMKE UNAYEDHANI ANAFAA KUIBUKA MSHINDI NA KUNYAKUA ZAWADI ZITAKAZOTANGAZWA BAADAYE: LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK (WWW.FACEBOOK.COM/GLOBALPUBLISHERS), KISHA PIGA KURA YAKO KWA ANAYEFAA AU
ANDIKA NENO WOMAN, KISHA ACHA NAFASI ANDIKA HERUFI ZA MWANZO ZA MAJINA YA MSHIRIKI, MFANO AK (KWA KUMCHAGUA ANNA KILANGO) KISHA TUMA KWENDA NAMBA 15564
IMETOLEWA NA GLOBAL PUBLISHERS LTD
No comments:
Post a Comment