Wednesday, October 2, 2013

ZIARA YA DK SLAA NCHINI MAREKANI


Dk. Slaa akionyeshwa jinsi mitambo ya kisasa inayotumika katika mafunzo inavyofanya kazi. Hii karakana ndiyo inayotumika kuwatayarisha vijana kuwa wabunifu na kuweza kijiajiri.
Dk. Slaa akitizama kwa umakini jinsi mitambo hii ya kisasa inavyofanya kazi.
Dk. Slaa wakati akipokelewa na viongozi wa Chuo Kikuu cha Central Piedmont.
Mitambo maalum inayotumika katika mafundisho ya viwandani. Hii ni kwa ajili ya kuwafundisha wanafunzi wanaochukua kozi ya kuendesha mashine viwandani.
Dk. Slaa pamoja na viongzi wa juu wa Charlotte Chamber of commerce kwenye picha ya pamoja baada ya kufanya maongezi ya ushirikiano wa kibiashara.
LEO asubuhi Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa aliyekuwa Washington DC ameelekea jimbo la North Carolina ambako amelakiwa na Rais wa Chuo cha Piedmond Community College chenye jumla ya campuses 16 na jumla ya wanafunzi 85,000.
Piedmont Community College ndiyo moja ya Community colleges bora zaidi Marekani, na imekuwa ikitayarisha wanafunzi mahiri kwenye eneo la Engineering.
Lengo kubwa la kiongozi huyu maarufu nchini kukutana na Rais wa Chuo, ni kujifunza siri ya mafanikio ya chuo hicho, kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi wa Kitanzania kufanya vizuri zaidi kwa lengo kubwa la kutayarisha rasilimali watu. Dk. Slaa pamoja na Chadema, wanaamini kwamba, ili kuliokoa taifa, lazima elimu ipewe nafasi ya kwanza
Kadhalika, Dk. Slaa na Rais wa chuo hicho,  walikubaliana kuanzisha programu maalum itakayowawezesha vijana wa Kitanzania na Wakimarekani kuanzisha urafiki utakaowezesha chuo hicho maarufu kufanya kazi kwa ukaribu na vyuo vya Tanzania. Vyuo vya Tannzania vitanufaika zaidi hasa kutokana na technolojia ya kipekee ambayo hipo chuoni hapo.

No comments:

Post a Comment