MSHIRIKI mmoja wa Shindano la Vigori 2013, anatarajia kutangazwa kuwa mshindi wa shindano hilo maarufu kwa mabinti kuzungusha nyonga vilivyo litakalofanyika Desemba 8, mwaka huu (Jumapili ijayo), katika Ukumbi wa Letasi Lounge, Victoria jijini Dar kuanzia saa 2 usiku.
Akizungumza na mwandishi wetu katika mahojiano maalum, mratibu wa tamasha hilo, Maimartha Jesse, alisema mshindi atakayepatikana, atazawadiwa gari aina ya Nissan March yenye thamani ya Sh. Mil. 8 ambapo mbali na shoo kali ya washiriki wa shindano hilo, mastaa kibao wa Bongo Fleva na bendi watatumbuiza.
Bendi zitakazotumbuiza ni pamoja na Sky Light, Exra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’ na Mapacha Watatu. Kwa upande wa Bongo Fleva, watakuwepo Makomandoo, Cankaranga (THT), Snura, Amini na Barnaba.
Kwa upande wa majaji, watakuwepo Elizabeth Michael ‘Lulu’, Gea Habibu, Martin Kadinda, Petty Money, Linah, John Kitime, Ally Lamtula na Maimartha mwenyewe.
Vigori saba wanaowania zawadi hiyo ya gari ni Neema Danford, Suzan Daniel, Monalisa Ivan, Amina Tafawa, Shuu Ndae, Mariam Ramadhani na Brigita Morice.


No comments:
Post a Comment