Monday, April 28, 2014

TBL YAPATA TUZO YA MAPAMBANO DHIDI YA MALARIA NCHINI‏

 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (kulia) akimkabidhi Meneja Vipaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Lillian Makau cheti cha shukurani cha kutambua ushiriki wa kampuni hiyo katika mapambano dhidi ya Malaria nchini, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati ni Balozi wa Malaria Tanzania, Leodegar Tenga.
 Katibu wa Afya wa TBL (katikati), akitoa maelezo jinsi kampuni yake ilivyojidhatiti kutoa elimu na tiba ya malaria kwa wafanyakazi pamoja na wananchi.
 Wananchi wakiwa katika sherehe za maadhimisho ya hayo kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, Dar es Salaam.
Makau akielezea mikakati ya TBL ya kuisaidia jamii na wafanyakazi katika mapambano  dhidi ya Malaria.
 Wageni waalikwa wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani.
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid, akitoa pongezi kwa Meneja Vipaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Lillian Makau (kulia) jinsi kampuni yake inavyoshiriki katika mapambano dhidi ya malaria kwa kuisaidia jamii na wafanyakazi wake, alipotembelea banda la TBL wakati wa maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani, Dar es Salaam jana. Katikati ni Katibu wa Afya wa TBL, James Lyimo. Wa pili kulia ni Meneja Uhusiano wa TBL, Editha Mushi.
 Katibu wa Afya wa TBL, James (kushoto) akijadiliana jambo na Meneja Uhusiano wa TBL, Editha Mushi wakati wa maadhimisho hayo.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa taasisi mbalimbali zinazoshirikiana na serikali katika mapambano dhidi ya Malaria nchini. Mstari wa mbele kutoka kulia ni Athuman Mfutakamba, Waziri Dk. Rashid  Balozi wa Malaria nchini, Leodgar Tenga.
(PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

No comments:

Post a Comment