Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia tiketi ya CCM, Ndugu Ridhiwani Kikwete akihakiki taarifa zake kabla ya kupiga kura kwenye kituo cha Ofisi ya Mtendaji Kata namba 3 Bwilingu, Chalinze.
Aziza ambaye ni mtoto wa mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia CCM, Ndugu Ridhiwani Kikwete akimsaidia baba yake kuweka kura kwenye sanduku la kura. Ridhiwani alipigia kura yake kwenye kata ya Bwilingu.
Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chadema, Ndugu Mathayo Torongey akizungumza na baadhi ya mawakala alipotembelea kituo cha Ofisi ya Mtendaji Kata namba 1, Bwilingu.
Mkurugenzi wa Uchaguzi Jimbo la Chalinze, Ndugu Samuel Salianga akizungumza na waandishi wa habari nje ya kituo cha Ofisi ya Mtendaji Kata Bwilingu na kutoa tathmini ya jinsi zoezi linavyoendelea na kufafanua mambo mbalimbali yanayohusu uhalali wa wagombea kupiga kura popote ndani ya jimbo la uchaguzi.
(PICHA ZOTE NA FATHER BLOG)
No comments:
Post a Comment