Zipo Make Up za kila aina zinazoendana na ngozi ya mteja ambapo pia unaweza kupata kwa bei Jumla na reja reja. Pichani wageni mbalimbali wanaopenda urembo wakiangalia Make up wakati wa uzinduzi huo uliofanyika kwenye Duka la Atsoko Beauty and Cosmetic lililopo Mikocheni jijini Dar.
Amesema kwamba ameamua kumchangua (Sing Bird) Shaa kama balozi wake kwa sababu ni mtu anayeweza kuwakilisha vyema kwenye sanaa kutokana na mavazi, muonekano na uelewa wake mkubwa katika mambo ya mitindo hapa nchini.
Mahimbo alisisitiza kwamba tukio hilo la Jumamosi iliyopita imetoa nafasi kwa wateja wake wa ndani na nje ya nchi kuweza kuona collection yake mpya ya 2014 hasa khanga na jeans.
Mtaalamu wa kucha katika Duka la Atsoko Beauty and Cosmetic Maryciana Naivasha akiwasikiliza wateja waliofika duka hapo.Katika tukio hilo alishirikiana Atsoko wa duka la vipodozi kuandaa ‘Face of Summer 2014’ katika kuwapa watu waliotembelea nafasi ya kuona kazi zake mpya za sanaa ya ubunifu, amesema
Shaa alichaguliwa kuwa balozi wa tukio hili na waandaaji kutokana na kuwa na sifa ambazo wao walizihitaji. Vida Mahimbo, Shaa, Rio Paul na Mary.Kwa sasa wateja wa nchini wataweza kupata bidhaa ya T-shirts Khanga na Jeans katika duka la Atsoko Beauty and Cosmetics zilizotengenezwa na Vida Mahimbo.
MBUNIFU wa mavazi Vida Mahimbo wa jijini Dar es Salaam Jumamosi ya wiki iliyopita amezindua ‘Collection’ yake ya ‘Face of Summer 2014’ yenye muonekano wa rangi za kimataifa.
“Nimekuwa kwenye tasnia ya mitindo na mavazi kwa takribani miaka minne na leo nimezindua ubunifu mpya wa mavazi inaoendana na rangi za kimataifa hasa kwenye T-shirts na jeans,” amesema Mahimbo
Mahimbo amesema kwamba yeye ana tengeneza nguo hasa za kike lakini ambazo zinaweza kuvaliwa karibu kila siku na watu wa rika mbalimbali wa kimataifa na watu wa kawaida.
(Picha na Zainul Mzige, MOblog).
No comments:
Post a Comment